Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa haitegemei kufutiwa udahili kwa wanafunzi kwenye  baadhi ya vyuo, kutawakosesha baadhi ya wanafunzi watarajiwa nafasi au kozi walizodhamiria kwenda kuzisoma.
Ofisa Habari Mwandamizi, Edward Mkaku ameyaeleza hayo kwenye Viwanja vya Maonesho, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana, na kusema kuwa TCU haitahusika na wanafunzi watakao kosa vyuo kwani kwa sasa wameratibu udahili na hivyo ni jukumu la mwanafunzi kutafuta chuo kulingana na ufaulu alionao.
“Hatutarajii mwanafunzi kukosa chuo, na pia kufutiwa udahili kwa baadhi ya vyuo siyo sababu ya wanafunzi kukosa nafasi kwenye vile vyuo vilivyopo,” alisema.