Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wasafi Cl;assic Baby (WCB) Rayvanny amefanikiwa kufikia rekodi ya juu  baada ya wimbo wake wa ‘Tetema’ video  yake kutazamwa mara milioni moja kabla ya masaa 24 katika mtandao wa Youtube.

Wimbo wa Tetema aliomshirikisha boss wake, Diamond Platnumz ,ulifanikiwa kutazamwa mara milioni moja kwa muda wa masaa 17 tu kabla ya masaa 24.

Wanamuziki Diamond Platnumz na  Alikiba ni baadhi ya waliofanikiwa nyimbo zao kutazamwa mara milioni moja kwa muda wa masaa 24.  Mpaka wakati huu wimbo huo umetazamwa mara milioni 1.2.