Idadi ya vifo imeongezeka hadi kufikia watu 12 na wengine 134 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 katika vipimo vya Richter lililotokea nchini China.

Zaidi ya watu 4,000 walihamishwa kutoka makazi yao kutokana na idadi kubwa ya majengo kuharibika au kuporomoka kabisa kufuatia tetemeko hilo la jana nje kidogo ya mji wa Yibin katika jimbo la Sichuan.

Matetemeko ya ardhi hupiga mara kwa mara katika jimbo la Sichuan, ambapo tetemeko kubwa la kipimo cha Richter 7.9 lilisababisha watu 87,000 kupoteza maisha yao au kutojulikana walipo mwaka 2008.