Leo July 4, 2019 Kumekuwa na tetesi kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye ni mwekezaji wa timu hiyo Mohammed Dewji amejiondoa kama Muwekezaji kwenye Klabu hiyo. 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji amesema, “watu wenye nia mbaya. Kazi yao sio kujenga, ni kuvunja tu. Kaa nao mbali. Narudia kaa nao mbali sana!”.