TFF yakanusha taarifa zinazo sambaa kuhusu kipa wa Yanga

Shirikisho la soka nchini (TFF), limesema taarifa zinazosambaa kuwa kamati ya hadhi za wachezaji ya TFF, imeidhinisha kuwa kipa wa Yanga Beno Kakolanya ni mchezaji huru kutokana na kuidai Yanga, si za kweli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Disemba 3, 2018 imeelea kuwa kamati hiyo haijaketi hivi karibuni na wala hakuna shauri la Kakolanya lililowasilishwa katika kamati hiyo.

”Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji haijakaa kupitia suala hilo kwahiyo taarifa hizo ni za uongo na zinasambazwa na watu wachache kwa maslahi yao’‘, imeeleza taarifa hiyo.

Mtibwa Sugar wakumbana na kibarua kizito kusaka taji kombe la shirikisho barani Afrika

Kakolanya amekuwa na sintofahamu na klabu yake ya Yanga kutokana na kutoonekana kwenye kikosi hicho tangu alipotoka nchini Lesotho alipokuwa na timu ya tiafa kwenye mchezo wa kufuzu AFCON.

Taarifa iliyosamba ilieleza kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji imeidhinisha kuwa Kakolanya ni mchezaji huru kutoka na kuidai Yanga mshahara wa miezi miwili pamoja na fedha za usajili.