TFF yaunda kamati kusimamia soka la Zanzibar

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limeteua kamati mpya  ndogo ya wajumbe 10 watakao simamia soka la Zanzibar kwa muda mfupi.

Akizugumza na Wandishi wa Habari Raisi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia amesema kamati hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia upatikanaji wa Katiba ya ZFA, na chaguzi ndogo za wilaya na kusimamia mashindano ndani ya ZFA.

Aidha karia amesema kamati hiyo wameiUnda baada ya vikao vya muda mrefu baina ya pande zote na kupata muafaka wa TFF kuunda kamati hiyo ambayo itafanya kazi zake hadi Novemba 30 mwaka huu.

Kuhusu suala la kamati ya iliounda mrajisi wa vyama vya michezo Karia amesema kamati hiyo kwa sasa haitofanya kazi tena baada ya TFF kuteuwa kamati hiyo ndogo na mazungumzo baina ya TFF na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar yalifanyika.

Kamati hiyo imeundwa na wajumbe kumi ambao ni Mwalim Ali Mwali (Mwenyekiti), Mohamed Ali Hilali(Katibu), Ahmada Haji Shaabani (Mjumbe) , Rashidi Tamimu Khalfan( mjumbe), Ikram Omar Sleman( mjumbe), Salum Ubwa Nassor (Mjumbe), Rajabu Juma Mtumweni (Ujumbe), Mzee Ali Abdalla (mjumbe), Khamisi Abdalla Saidi(Mjumbe)na Mzee Ali Mzee (Mjumbe).

Kwa upande mwengine taarifa kutoka kwa kamati teule kwa niaba ya kamati hiyo kamati ya mashindano na kamati ya Club Lesense itandelea kufanya kazi kama kawaida.