Timu Hizi Hapa Tushio Msimu Ujao Wa Ligi Kuu Ya Zanzibar 2018/2019.

Wakati wadau wa mpira wa miguu Zanzibar wakisubiri kwa hamu kuona msimu ujao wa ligi kuu ya Zanzibar ambao utachezwa kwa mkondo mmoja kwa pamoja baada ya miaka minne ya kuchezwa kwa mfumo wa kanda unguja na pemba.

Kwa sasa kwa mujibu wa kalenda ya chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) ipo katika dirisha la usajili kwa madaraja yote na ngazi zote.

Katika makala hii mpenzi msomaji wa blogi ya Zanzibar24 nitakuletea timu ambazo tishio kwa msimu ujao wa ligi kuu ya Zanzibar ambao utakuwa na timu 20.

JKU SC.

Mabingwa watetezi mara mbili mfulilizo wa ligi kuu ya Zanzibar wana rikodi nzuri sana kwa misimu hii ya karibuni kwa kufanya vizuri sana kwenye mashindano ya kimataifa na ile rikodi ya ligi kuu ya Zanzibar ya muda mrefu kwa uzoefu wao.

Wanawachezaji wazoefu sana licha ya moja ya timu ambazo zimetoa wachezaji wengi timu ya Taifa ya Zanzibar ni dalili za wazi kuwa Jku ni moja tishio kubwa msimu ujao na kwa mujibu wa kikosi chao hawahitaji usajili wa wachezaji wengi kwa kuwa wanajivunia kuwa na wachezaji kama vile Issa Haidar (Mwalala), Bopa,Nassor Matar, na wengine wengi wenye uzoefu mkubwa sana.

Tishio lao kubwa wanangia kwenye ligi kuu ya Zanzibar msimu huu wakiwa wanatarajia kuwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa ya CAF, na msimu uliopita hatua ya nane bora wamepoteza mchezo mmoja tu.

ZIMAMOTO SC.

Timu yenye bahati inayoundwa na benchi la ufundi la kawaida sana lakini imekuwa ikijua mbinu nyingi za kupambana ili kupata ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar.

Msimu unaokuja Zimamoto huenda ikawa tishio kwa timu nyengine kwa kuwa inaundwa na vijana wazoefu wa kuuchezea mpira na mashindano makubwa ya kimataifa.

Zimamoto iliwahi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka 2015 /2016 chini ya mkufunzi Abdalla Bares sasa klabu hiyo ipo katika uimara zaidi huenda ikawa tishio msimu ujao wa ligi kuu ya Zanzibar kwa aina ya usajili watakao ufanya ikiwemo kumrudisha kinara wao Simba Ibrahim Hamada Hilika ndani ya kikosi chao ili kuimarisha nafasi ya ushambuliaji.

Malindi .(PSG)

Ni timu iliyopewa jina la timu moja barani ulaya inayotoka ndani ya Ufaransa PSG kutokana maandalizi yake makubwa walioyafanya licha ya mgogoro mdogo uliotokea ndani ya klabu hiyo lakini imeweza kujiimarisha kuanzia safu ya uongozi hadi benchi la ufundi kwa kuhakikisha wanatengeneza timu ya ushindani ndani ya klabu hiyo.

Hii itakuwa tishio msimu ujao kwa kuwa wamewekeza kwenye usajili wa mkubwa zaidi ikiwemo kusajili wachezaji wengi wenye kiwango cha juu na uzoefu ndani ya ligi kuu ya Zanzibar.

Malindi wamekuwa na malengo makubwa ya kuhakikisha wanachukua taji la ligi kuu ya Zanzibar msimu huu hivyo itakuwa ni tishio kubwa ndani ya msimu unaofata wa ligi kuu ya Zanzibar , wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa Zanzibar Heros Khamisi Mussa Raisi, kiungo wa Abdul Swamad KassimGuti kutoka Stand United, mlinda mlango machachari Ahmed Ali Salula, na wachezaji wengi ambao imekuwa chachu ya timu hiyo kutarajia kupata mafanikio zaidi safarini.

Jang’ombe Boys.

Wanaitwa wastarabu wa ng’ambo moja ya timu ambazo zina jina kubwa sana na tishio kwa msimu ujao wa ligi kuu ya Zanzibar, imekuwa ikifanya maajabu makubwa wakiwa uwanjani licha ya kuwa na wapenzi wengi lakini wamekuwa wapinzani wakubwa wa Taifa ya Jang’ombe.

Ni timu yenye bahati sana ilifanikiwa kufuzu hatua ya nane bora msimu mmoja na kufanikiwa kucheza mashindano ya kimataifa ,ndo timu ya kwanza kuifunga klabu ya URA kutoka Uganda kwenye mashinadano ya Mapinduzi Cup mwaka 2017 baadae Taifa ya Jangombe ikawa timu ya pili na Jamuhuri ya pemba nayo ilifanikiwa kuifunga URA kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup.

Mwaka huu huenda ikawa tishio msimu unaofuata kwa kuwa wamejiapanga kwenye usajili si wa kawaida baada ya kuinasa saini ya aliyekuwa mshabuliaji wa Tanzania Prisons ya jijini Mbeya na Timu ya Taifa ya Zanzibar Heros Kassim Suleiman Khamis hii inaweza kuamsha hamasa kwa klabu hiyo na kuwa na timu bora yenyekueweza kuleta ushindani ndani ya msimu huu.