Timu ya soka la ufukweni Zanzibar yajipanga na mechi dhidi ya Timu ya Taifa Tanzania bara

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni kinaendelea na mazoezi katika viwanja vya Ufukwe wa Bububu Zanzibar kwa lengo la kujiandaa na mechi dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania bara kwalengo la kutafuta timu ya Taifa ya soka la ufukweni Tanzania itakayo kwenda kuchuana katika mashindano ya Afrika.

Akizungumza na Zanzibar24 Kocha mkuu wa Timu hiyo Ali Sharifu Adofu amesema timu hiyo ipo muda mrefu mazoezini na kambi ya muda kwa lengo la kuleta ushindani kwenye mechi hizo mbili .
Aidha amesema timu hiyo bado inachangamoto kubwa ikiwemo fedha za kuendesha timu hiyo zimekuwa ni haba hususan posho za wachezaji, “Tumeshapeleka taarifa kwa kamati iliYoteuliwa na tunaendelea kushirikiana nayo japo kuna changamoto nyingi kwenye timu yetu ila tuko vizuri kiushindani” Alisema Adofu.
Kuhusu suala la mashindano ya CECAFA ya soka la ufukweni Adofu amesema kwa sasa timu hiyo bado ipo kwaajiili ya mashindano hayo na tayari timu ya Taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni ipo muda mrefu sana.