Timu za vikosi zinaendelea kutesa ligi kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora baada ya klabu ya KVZ kuiyangushia kichapo cha mbwa mwitu klabu ya Opec kwa magoli saba kwa bila kwenye uwanja wa Amani mjini Unguja kwenye mzunguko wa sita wa ligi kuu ya Zanzibar.

Kwa Upande wa Zimamoto wamefanikiwa kuondoka na alama tatu baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Mwenge magoli moja kwa bila na kuongoza ligi hiyo.

Msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar kwa sasa unasomeka kwa Upande Zimamoto ndie kinara wa ligi kuu ya Zanzibar akiwa na alama 13,akifuatiwa na Kvz mwenye alama 12,na Jku wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 9 na klabu ya jamuhuri wakiwa na alama 5 wakiwa nafasi ya nne.

Kwa Upande Dimba la Gombani michezo ya ligi kuu ya Zanzibar itachezwa kesho Jku dhidi ya Jamahuri na Mafunzo dhidi ya Hardrock.