Rais wa Marekani Donald Trump ameomba kurejewa kwa kuisabiwa kura akitaka sehemu ya kura za Jimbo la Wisconsin huku Timu yake ya Kampeni ikidai kuna mapungufu katika Kaunti za Milwaukee na Dane

Maombi hayo yanasema kuwa kuna udanganyifu umefanyika katika kura zilizopigwa kwa njia ya posta japokuwa hawajatoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao

Kwa Sheria za Jimbo hilo, Rais Trump ana haki ya kuomba zoezi hilo lirudiwe, lakini ametakiwa kugharamia mchakato ambapo Maafisa wamesema tayari wamepokea Dola za Marekani Milioni 3 kutoka Timu ya Kampeni ya Trump.