Kufuatia tuhuma zinazomkabili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Juventus kutoka Italia Cristiano Ronaldo za kumbaka mwanadada mmoja nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Kathryn Mayorga.

Ronaldo ameamua kujitoa kwenye kikosi cha timu ya taifa katika mechi mbili zinazofuata ambazo ni kati ya Poland pamoja na Scotland.

Kathryn Mayorga mwenye umri wa miaka 34 inadaiwa alibakwa na Ronaldo mnamo mwaka 2009 nchini Marekani na Ronaldo inasemekana alimlipa millioni 794, Ingawa mchezahi huyo amekanusha vikali madai hayo.

Ronaldo ataukosa mchezo wao dhidi ya Poland katika michuano ya UEFA Nation League ambao utafanyika mwezi Octoba tarehe 11 huku siku tatu baadaye wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Scotland.