Tukio la Tundu Lissu kushambuliwa na watu wasiojulikana lachukuwa sura mpya

Mbunge wa Singida Mashariki kwa upande wa Chadema, Tundu Lissu ameanza rasmi ziara maalum katika bara ulaya kwa lengo la kueleza tukio la yeye kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo mwezi Septemba 2017.

Tundu Lissu ameanza ziara yake hiyo nchini Uingereza na kisha atakwenda nchini Marekani.

Mwanasheria huyo Mkuu wa CHADEMA anatarajia kutumia ziara yake hiyo kueleza tukio la kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Utakumbuka Septemba 17, 2017 Tundu Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi akitokea Bungeni Jijini Dodoma ambapo alipatiwa matibabu ya mwanzo nchini Kenya kisha kuhamishiwa Ubelgiji.