Tunda ‘the Boss babe’ asikitishwa na yanayo mkuta Amber Ruty

Video Vixen wa Bongo Fleva, Tunda ‘the Boss babe’, amemuombea msamaha  Amber Ruty, kutokana na yale anayoyapitia katika maisha yake hivi sasa.

Akizungumza na Big Chawa wa East Africa Radio, Tunda amesema amemuomba Mungu awasamehe Amber Ruty na wengine, kwani hawajui walitendalo, huku akiwataka na watu wengine kuwahurumia vijana hao kwakuwa wanapitia kipindi kigumu.

Tunda
 ‘the Boss babe’ ‘kushoto’ akiwa na 
Amber Ruty

“ Eeh Mungu Samehe wote pamoja na vizazi vyetu, hawajui walitendalo, kwa Amber Ruty siwezi kusema kitu, kwa sababu sijui mazingira gani yalitokea kwake, inawezekana hata yeye yupo kwenye wakati mgumu, au hakupenda itokeee vile”, amesema Tunda

Tunda ameendelea kwa kusema kwamba sheria zilizopo nchini hivi sasa zimemfanya awe muoga wa kufanya vingi, ikiwemo  kujirekodi akifanya  alichokiita ‘upumbavu’ 

Ikumbukwe kwamba siku za nyuma zilishawahi kuvuja video zikimuonyesha Tunda akiwa faragha na mmoja wa mtoto wa kigogo hapa nchini, ambapo baadaye mwenyewe alijitokeza hadharani na kuomba msamaha.