Muandishi wa Habari kutoka Zanziba24 akipokea tunzo
bora ya Uandishi wa Makala na habari tofauti zinazohusiana na Rushwa na Uhujumu Uchumi katika ngazi ya uandishi wa Habari za TV.

Mamlaka ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ZAECA yatoa tunzo bora ya Uandishi wa Makala na habari mbali mbali zinazohusiana na Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo Muandishi Tatu Juma kutoka Zanzibar24 ameinyakua nafasi ya pili katika kinyan’ganyiro cha uandishi wa Habari za TV.

Tunzo hizo zimeshindaniwa na waandishi mbali mbali Visiwani Zanzibar na zimewashirikisha waandishi katika nafasi Tatu, Uandishi wa Habari wa Magazeti, Uandishi wa Habari za Redio na Uandishi wa Habari za TV,

Waandishi wengine waliopata Tunzo hizo ni pamoja na Ameir khalid kutoka Zanzibar leo Mtandaoni,Salum Vuai kutoka Wizara ya Habari, Asha hamadi kutoka Chuchu FM Redio pamoja na Habiba kutoka Zanzibar leo.

Hafla hiyo ya utoaji wa Tunzo kwa waandishi wa habari ilifanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbeni Mjini Magharib na Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na utalawa bora Zanzibar Haroon Ali Suleimani.