Maafisa wakuu wa Urusi na Marekani wamejibizana baada ya ndege mbili kubwa za kuangusha mabomu za Urusi kutua nchini Venezuela, taifa linalopatikana Amerika Kusini.

Ndege hizo mbili zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.

Ndege hizo za kivita aina ya Tu-160 zilitua Venezuela Jumattau katika kile kinachoonekana kama jaribio la kuonyesha uungaji mkono wa Urusi kwa rais wa Kisoshialisti wa Venezuela Nicolás Maduro ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kitendo hicho ni sawa na “serikali mbili fisadi kufuja mali ya umma.”

Serikali ya Urusi imesema maneno yake hayo “hayafai hata kidogo.”

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Ndege hizo mbili za kivita zenye uwezo wa kusafiri mwendo mrefu bila kutua zilitua katika uwanja wa ndege wa Simón Bolívar viungani mwa mji mkuu wa Venezuela, Caracas, zikiandamana na ndege nyingine mbili za Urusi.

Venezuela na Urusi zimekuwa marafiki kwa muda mrefu na ndege hizo mbili za kivita ziliwahi kutumwa tena taifa hilo mwaka 2008, zikiwa pamoja na manowari moja yenye uwezo wa kurusha makombora.

Ndege hizo zilifika tena Venezuela mwaka 2013.

The arrival of two Russian Tupolev Tu-160 strategic long-range heavy supersonic bomber aircrafts at Maiquetia International Airport, just north of Caracas, on December 10, 2018.
Image captionWaziri wa ulinzi wa VenezuelaVladimir Padrino (wa pili kushoto, mstari wa mbele) aliwalaki Warusi hao

Kitendo cha sasa kimetokea siku chache tu baada ya rais Maduro kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow.

Waziri wa Ulinzi wa Venezuela Vladimir Padrino alisema ndege hizo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Venezuela na mshirika wake Urusi.

“Hili tunalifanya kwa pamoja na marafiki zetu, kwa sababu tuna marafiki duniani ambao hutetea na kuheshimu uhusiano wa usawa.”

Chanzo BBC Swahili.

Presentational grey line