Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umewashauri raia wake kurejea Marekani, kufuatia uwepo wa maambukizi ya virusi vya COVID19

Ubalozi umewataka raia wake wote wanaotaka kuondoka kufanya hivyo mapema kutokana na mashirika mengi ya ndege kusitisha safari hadi kufikia Machi 29, 2020 Shirika la Ndege pekee litakalokuwa na ndege za kutoka nje ya Tanzania ni Shirika la Ethiopia

Ubalozi huo umesema kwa sasa haushughuliki na kuwatoa raia hao nje ya Tanzania kuwarudisha Marekani, ila kama hatua hiyo itafikiwa umewataka wale wote watakaotaka kutafutwa na Ubalozi huo kutuma taarifa zao muhimu za utambulisho