UCHAMBUZI WETU: Nane bora ligi kuu Zanzibar ilete utafaouti kiushindani

Hatua ya Nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar inatarajiwa kuanza rasmi baada ya mapumziko mafupi na kumalizika hatua ya kanda ya Unguja na pemba ambayo kwa mujibu wa kanuni ya ZFA ya mashindano imekuja baada ya chama hicho kutokuwa na mdhamini wa kundesha ligi kuu ya Zanzibar.

Hatua hii muhimu ya Nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar inaonekana kwa baadhi ya wadau wa mpira wa Zanzibar haileti ushindani wa hususan vilabu vinavyotoka upande wa pili wa kisiwa cha pemba vinatoka uraiani vinashindwa kujiendesha na kusababisha kuzorota kwa hatua hii muhimu ya Nane bora ya ligi kuu Zanzibar(ZPL).

Mandalizi ya vilabu hivi vinavyoshiriki hatua hii muhimu ya nane bora ambayo tunamtafuta Bingwa wa Zanzibar atakae iwakilisha  nchi kwenye mashindano ya kimataifa ya CAF ambayo kwa muda mrefu vilabu vyetu vimekuwa washindikizaji kwenye mashindano haya makubwa ya kimataifa.

Wadau wa michezo hususan wapenzi wa mpira wa miguu Zanzibar wanatarajia ushindani wa kimchezo katika hatua ya nane bora ya msimu huu ligi kuu ya Zanzibar bila ya kuwepo ubabaishashaji wa  vilabu  na upangaji wa matokeo wakati wa ligi kuu ya Zanzibar.

Lazima vilabu vijipange vizuri kuhakikisha vinaleta ushindani na kuwafanya wadau na wakereketwa kuja viwanjani kushuhudia ligi kuu ya Zanzibar ambayo kimsingi kwenye mioyo yao haina nafasi kwa mpira  wa Zanzibar  kilichobaki ni uzalendo tu  na kupenda cha kwetu.

Tunategemea viongozi waliopewa dhamana kusimamia hatua hii ya Nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar watakuwa wamejifunza mengi na kuepuka rushwa, upendeleo kwa baadhi ya vilabu ambavyo vinautaka Ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar bila ya kutumia bidii ya uwanjani kuonyesha kiwango kizuri.

Hatupendi kuona hatua hii muhimu ya ligi kuu ya Zanzibar inaonekana ni kituko kwa mpira wa Zanzibar kwa upangaji wa matokeo wa dhahiri na hata wa siri na utumiaji wa fedha kwa timu kutaka alama tatu ili kujitingenezea mazingira ya kuwa bora Bingwa sio Bingwa bora wa ligi kuu ya Zanzibar.

Malalamiko yalitokea hatua ya kanda kwa baadhi ya waamuzi kulalamikiwa kupendelea baadhi ya vilabu na rufaa zisizo za lazima kwa ZFA lazima yaonekane ilikuwa ni changamoto ambazo zinaweza kufanyia kazi na kuepukika kwenye hatua hii ya Nane bora ili kurejesha imani kwa wadau wa mpira wa miguu Zanzibar kwenye ligi yetu ya nyumbani Zanzibar .

Vilabu kama vile Mwenge, Jamuhuri, Opec vinaweza kubeba matumaini ya mpira wa Zanzibar kwenye hatua hii muhimu kama vimepata matayarisho ya kutosha na mandalizi ya Nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar kwa kuwa ndio vilabu vilivyopo uraiani ambavyo vipo chini ya wananchi ambao ndio wanaoguswa na mpira wa Zanzibar  kwa muda mrefu sana.

Tuhahitaji ushindani mkubwa kwenye hatua hii ya nane bora na kuondosha dhana ya kuwa vilabu vya Unguja pekee ambavyo vinaweza kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar, hivyo wadau wa mpira wajitokeze kwa wingi kuja kuunga mkono mpira wetu zanzibar, turudi kwenye mpira wetu ili tuwakaribishe wadhamini.

Na: Ibrahim Makame Zanzibar 24.