UCHAMBUZI WETU : Tuiyunge mkono zaha mwenyeji wa mashindano ya mpira wa mikono afrika mashariki mwezi Disemba

Kwa mara ya kwanza chama cha mpira wa mikono Zanzibar ZAHA kinapokea kijiti cha kuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa mikono Afrika Mashariki na kati sio jambo la kawaida ni jambo la kupigiwa mfano kwa tasisi ndogo kama ZAHA ya kubeba mashindano makubwa kama haya.

Kwa muda mrefu Zanzibar tumekuwa na historia nzuri kwa upande wa michezo licha ya changamoto kubwa ya vifaa na fedha za kuendeshea michezo yetu lakini kunahaja ya kujipa hongera  kuwa kuwa visiwa vyetu ni vya lulu ya michezo mingi sana ambayo huchezwa Zanzibar.

Dawati la michezo Zanzibar 24 tunakipa hongera sana chama cha mpira wa mikono Zanzibar chini ya uongozi wake mwenyekiti Salum Hassan Salum na Katibu wake Mussa Abdulrabi Fadhil kwa jitihada mbali mbali za kutaka kuukuza mchezo wa mpira wa mikono Zanzibar licha ya kuonekana mchezo huo hauna kasi visiwani hapa.

Zanzibar ni asili ya vipaji vya michezo kwa muda mrefu sana Zanzibar imekuwa ikipiga hatua kila siku na mabadiliko ya michezo kwenye Nyanja tofauti,kwa upande wa mpira mikono Zanzibar tumebahatika kuwa na wachezaji wengi wanaounda timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo huo na bahati ya pekee kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ni mzanzibar ndugu Kombo Ali Kombo.

Hatuna budi kuwaunga mkono ZAHA kwa jitihada kubwa ya kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo yatakayo husisha takribani nchi tano za Afrika Mashariki ikiwemo na DR C kongo ni moja ya chachu kubwa ya kutangaza nchi yetu kwenye mashindano haya ya Afrika Mashariki.

Kwa umoja wetu baina lazima tuiyunge mkono ZAHA kila mwenye mchango wake kuanzia udhamini ,matangazo vyombo vya habari kuripoti kwa wingi mashindano hayo hata serikali wanawajibu mkubwa kuhakikisha wanatoa mchango mkubwa ili kufanya mashindano hayo kuwa na hadhi ya kimataifa kwa kuwa Zanzibar tupo kwenye kipindi kizuri kwenye sekta ya michezo.

ZAHA imekuwa kila baada ya miezi mitatu huendesha Clinic maalum ya mchezo wa mpira wa mikono ambayo tunatarajia baada ya kipindi kifupi matunda ya clinic hizi yataonekana kwa kuwa vijana wadogo ndio wanaopewa mafunzo ya Clinic hizi.

Dawati la Zanzibar 24 tunaipongeza ZAHA kwa jitihada kubwa ya kuhakikisha wanakuza mchezo huo wito wetu ni kuhakikisha wanajindaa kuleta ushindani wa katika mashindano hayo ya Afrika Mashariki na Ubingwa wa mashindano hayo kubaki Zanzibar kwa jinsia zote wanawake na Wanaume.

Tunaamini bado mnachangamoto kubwa ya kuleta mafanikio hivyo wadau wa michezo na wafanya biashara ni fursa pekee hiyo kwa Zanzibar kuhakikisha mnatumia mashindano hayo kutangaza biashara zenu kwa kuwa mchezo wa mpira wa mikono huchezwa viwanja vya wazi hivyo huleta tija kubwa sana kama tutalia mkazo mashindano hayo.

NA Ibrahim Makame Zanzibar 24.