Uchungu wa mwana aujuae mzazi ,Wenye kuyabeza mapinduzi wachukuliwe hatua za kisheria

Wazee wa Jumuiya ya Wazee Zanzibar wameiyomba Serikali ya Mapinduzi zanzibar ya awamu hii ya saba kusaidiwa  katika suala la matibabu kwani bado wazee wengi  wanasumbuliwa na magonjwa vitandani.

Wakizungumza katika hafla ya ufanyaji usafi katika maeneo ya makaburi ya Mwanakwerekwe  ikiwa ni shamrashamra ya kuelekea  katika  kilele cha Mapinduzi matukufu ya 1964 wamesema bado wazee wanasumbuliwa na maradhi licha ya kuwa serikali iliwaahidi kuwapatia bima za afya lakini bima hizo wanahisi hazitasaidi kutokana wazee waliowengi wapo vitandaji hawananguvu za kufika katika kituo vya afya.

Hivyo wameiyomba serikali kuwateuwa madaktari maalumu ambao wawewanapita kila baada ya muda katika sheria ambazo wazee wanaishi kwalengo la kutoa huduma za matibabu ili kuwaondolea usumbufu  wakufata  huduma hizo.

Wamesema wazee hao kipindi cha ujana wao walitoa mchango kwa kutumia nguvu zao  katika ujenzi wa taifa hasa katika shughuli za maendeleo kwenye jamii hivyo lazima na wao kuthaminiwa ili kuweza kufaidika na vitu walivyovichuma wakati wa ujana wao.

Aidha wamesema  miongoni mwa maradhi yanayowasumbua wazee hivi sasa ni maradhi ya viungo kama mgongo,miguu na sukari,presha na magonjwa mengine .

Hata hivyo wamesema mbali na tatizo la maradhi lakini pia wamemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein  kumteumwa  mwakilishi kwa ajili ya wazee atakae wasaidia kuwafikishia matatizo yao ndani ya vyombo vya sheria ikiwemo kwenye baraza la wawakilishi kwani kwakundi mengi mfano vijana,wanawake na watu wenye ulemavu tayari wanawawakilishi wao ukilinganisha na wazee hakuna.

Wamesema lazima ateuliwe mwakilishi ambae atawakilisha  kauli za wazee kwenye baraza la wawakilishi kwani hatua hiyo itasaidia  zaidi na kukumbuka kama wapo nao nchini.

Mapema Akitoa Wito kwa wananchi hasa vijana Msimamizi wa JUMAZA Hashim Bakari Kondo amewataka vijana  kuwacha tabia ya kuyabeza mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 kwani  ndio mkombozi wa maisha ya wazanzibar.

Kondo amesema  maendeleo yote yanayopatikana  hivi sasa yanatokana na mapinduzi ya 64 hivyo lazima yalinde na ataeonekana kuyabeza achukuliwe hatua za kisheria kwani bila ya mapinduzi wasingeweza  kutembea kifua mbele hivi sasa.

Amesema mapinduzi yamezaa matunda mengi ikiwemo elimu bila malipo,pencheni kwa wazee wa miaka 70,majumba ya maendeleo unguja na pemba,maji safi na salama,barabara pamoja na kupata uhuru wa kujitawala wazanzibar wenyewe.

Amina Omar