Uefa kuanzisha michuano mipya ya Soko

Shirikisho la soka barani Uefa linatarajia kuazisha michuano mingine mipya na ya tatu kwa ukubwa soka barani humo baada ya ile ya klabu bingwa ulaya na Europa ligi.

Kwa Mujibu wa mwenyekiti wa Muungano wa vilabu barani ulaya, Andrea Agnelli, michuano hiyo ya tatu kwa ukubwa inatarajiwa kuanza kuanzia mwaka 2021.

Agnelli amesema michuano itasaidia kuongeza vilabu vinavyoshiriki michezo ya ulaya kutoka 80 mpaka 96

Hata hivyo  hakufafanua muundo upi utatumika katika michuano hiyo mipya.

Wazo la kuanza kwa michuano hiyo kutaifanya michuano ya Europa ligi kupungua timu toka timu 48 mpaka 32. Hivyo michuano yote itakuwa na idadi sawa ya timu.