Ufilipino imerejesha tani za takataka nchini Canada, baada ya mvutano wa kidiplomasia wa majuma kadhaa ambapo Rais wa nchi hiyo Rodrigo Duterte kutishia ” kusafirisha takataka kwa njia ya maji kuelekea Canada”.

Ufilipino imesema takataka hizo ziliwekwa nembo kimakosa kuwa zilikua za plastiki tayari kwa kutengenezwa upya (recycling) zilipofikishwa Manila mwaka 2014..

”Baaaaaaaaa bye, tusemavyo,” Waziri wa mambo ya nje wa Ufilipino Teddy Locsin Jr aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Ijumaa asubuhi.

Makontena 69 ya takataka yalirejeshwa yakiwa kwenye meli ya mizigo kutokea ghuba ya Subic, kaskazini mwa mji wa Manila.

Waziri, ambaye amekua maarufu kwa mtindo wa kauli zake kwenye ukurasa wake, aliweka picha na video ya meli ikiondoka bandarini.