Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema atawaamuru polisi wa nchi hiyo na wanajeshi kupiga risasi mtu yeyote ambaye atasababisha fujo au vurugu wakati huu ambao shughuli za nchi zimesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja kuzuia maambukizi ya COVID-19 (Corona virus).

Akilihutubia taifa hilo siku ya jana Rais Duterte alisema “Wacha hii iwe onyo kwa wote. Ni muhimu kufuata maagizo yote ya serikali wakati huu kwa sababu ni muhimu, Na msiwadhuru wafanyikazi wa afya kwa sababu huo ni uhalifu mkubwa”.

“Maagizo yangu kwa polisi na wanajeshi, ikiwa mtu yeyote ataleta shida, basi maisha yake yapo hatarini Apigwe risasi.”