Zaidi ya watu 30 wa Wilaya ya Bududa wanahofiwa kufariki kutokana na kufukiwa na matope yaliyosababishwa na mafuriko kufuatia mvua kali ya saa 5 mfululizo

Mafuriko hayo yamesababisha kukithiri kwa matope katika vijiji vya Namasa na Naposhi na yaliripotiwa kuingia katika nyumba zaidi ya 20, mashambani na kusababisha Barabara nyingi kujaa maji jambo lililosababisha harakati za uokoaji kuwa ngumu

Mafuriko hayo yameathiri na kuvunja madaraja ya kuunganisha kaunti za Bubiita na Buwali, Halmashauri ya jiji la Buwali na Kwushu, Kaunti ndogo ya Bulucheke na Kaunti ndogo ya Bushiyi kuvuka Mto Manafa