Uongozi wa Jimbo la Pangawe umeahidi kushirikiana na Uongozi wa Skuli ya Msingi Kinuni ili kuondosha Idadi kubwa ya Wanafunzi madarasani.

Hayo yameelezwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Khamis Juma Mwalim wakati alipokuwa akikabidhi Matofali, Mawe na Saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabanda mapya ya Skuli hiyo.

Amesema Idani ya Wanafunzi Wanaosoma ni kubwa ambapo ni kati ya 150 hadi 250 kwa Darasa moja jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za Ufundishaji.

Amefahamisha kuwa kukabidhi Msaada huo ni kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuenua sekta ya elimu hapa nchini.

Aidha amewaomba Waalimu kusomesha kwa kufuata Mitaala iliwekwa na Serikali ili kuwezesha Wanafunzi kufanya vema Mitihani ya Taifa.

Takdir Ali