Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Conservatives nchini humo atakayechukua mara moja nafasi ya Bi Theresa May.

Hii inamaanisha Boris Johnson sasa atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya May kutangaza kujiuzulu mwezi uliyopita.
Boris aliye na miaka 55 alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa wanachama wa chama cha conservatives.

Waziri huyo wa masuala ya kigeni wa zamani wa Uingereza anatarajiwa kuchukua rasmi nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu leo Jumatano (24.07.2019).