Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameandika ujumbe mzito kwa Mtoto Wake aliyezaa na Zari The Bosslady Prince Nillan ikiwa ni siku yake ya kusheherekea kuzaliwa kwake.

Siku ya Leo Nillan anafikisha umri wa miaka miwili pamoja na kuwepo maneno Mengi kwenye mitandao ya kijamii tangu anazaliwa kuwa sio Mtoto wa Diamond lakini Diamond amesema siku zote ni Mtoto Wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amemuandikia ujumbe mzito mtoto wake huyo na kusema: Miaka miwili iliyopita Mungu alinibariki na Mtoto wangu wa kwanza wa kiume naye nilimuita jina la Nillan linalomaanisha Mwezi/ Asili/ Umaarufu/ Handsome na ni handsome kweli anayeng’aa zaidi ya nyota Happy Birthday Nillan Baba anakupenda”.