Waziri wa fedha na Mipango Dk.khalid Salum Muhamed amesema ukuwaji wa uchumi umekuwa kwa asilimia 6.8 katika mwaka wa fedha 2017/18 na kupelekea mapato kuengezeka kwa zaidi ya asilimia mia moja.

Akijibu hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  Chukwani nnje kidogo ya mji wa Zanzibar ,amesema ukuwaji huo unaiwezesha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuwahudumia wananchi katika sekta mbali mbali ikiwemo kwalipa wazee pencheni kwa kila mwezi pamoja na kuiwezesha serikali kuwalipa mafanya kazi wake kuanzia laki tatu kwa wafanyakazi wa kima cha chini.

Amesema ukuwaji huo unatokana na udhibiti wa mapato serikali ikiwemo kupunguzwa kwa safari za viongozi za nnje ya nchi ,kupunguza semini na mikutano isiyo na tija jambo ambalo linachangia kuengezeka kwa ukuwaji wa uchumi.

Kwa upande wake waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu Said sudi amewataka Wawakilishi kuunga mkono juhudi za seriali katika kuimarisha miradi ya Maendeleo  ili kwenda sambamba na ukuwaji wa Uchumi katika kuwahudumia wananchi.

Aidha amesema ni vyema kwa kamati  ya uchunguzi na udhibiti wa hesabu za serikali na mashirika P.A.C kuwatolewa taarifa wawakilishi wanaoshindwa kuwasilisha ripoti za mfuko wa jimbo ili serikali itambuwe namna ya fedha za jimbo zinavyotumika katika kuthibiti mapato ya serikali.

Amesema wakati umefika kwa Viongozi kufanya kazi kwa kuacha muhali ili kuimarisha uchumi kwa maslahi ya nchi na Wananchi katika kunufaika na mapato yanayopatikana.

Na:Fat-hiya Shehe Zanzibar24.