Ukweli kuhusu ugonjwa wa Kichaa cha Mbwaa

Ugonjwa wa kichaa cha Mbwa ni ugonjwa hatari unaoathiri ubongo na kwa kawaida unamuua aliyeambukizwa nao.

Ugonjwa huu unasababishwa na virusi wanaokwenda moja kwa moja kwenye mishipa ya fahamu na kusababisha uvimbe wa ubongo (encephalytis), Mara nyingi humpata mbwa ambaye akimtafuna mnyama mwengine aina ya Mamalia na kumtoa damu akimtia mate teari nae anampa  ugonjwa huo

Asilimia 99% za watu huambukizwa na mbwa. Lakini inatokea pia mara kwa mara kwa Paka, Mbweha, Mbwa mwitu, Ng’ombe, Kondoo, Farasi, Twiga, Nguruwe, Punda, Nyati, Tembo na pia wapo aina za ndege.

Njia za maabukizo ni mate na damu hasa kwa njia ya kung’atwa na mnyama mgonjwa. Watu wanaotibiwa mara moja baada ya kuambukizwa wanaweza kupona. Lakini tiba inahitaji kutekelezwa kabla virusi havijafika kwenye ubongo kwa hiyo katika muda wa masaa ya kwanza baada ya kung’atwa.

Ugonjwa huu huonesha dalili za maambukizo baada ya wiki 2 hadi miezi mitatu kutegemea na sehemu uliyotafunwa ipo karibu kiasi gani na mshipa wa fahamu (Ubongo, Uti wa Mgongo) na mara ya kuonesha dalili kinachofuata mgonjwa hato zidi siku tatu hupoteza maisha hivyo wataalamu wa afya hushauri mgonjwa kupatiwa matibabu ndani ya masaa 24 baada tu yakutafunwa ili kuokoa maisha yake awe mnyama au binaadamu.

Kuna aina mbili za kichaa cha Mbwa: kichaa baridi ambacho dalili zake ni kuparalaizi na kutokwa na mate. Kichaa moto dalili zake kwa mnyama ni kubadilika tabia kama kuwa mkali, kutafuna tafuna vitu ovyo, kukimbia kimbia ovyo, kutokwa na mate mengi.

Kwa upande wa Binaadamu dalili huwa ni kubweka kama Mbwa, kupiga kelele, kutafuna vitu, kuogopa maji na mwangaza, kutokwa na mate ambapo waathirika hawa wote wanapomtafuna mtu wakimtoa damu na kumtia mate basi nae huambukizwa.

Ugonjwa wa kichaa cha mbwa unapatikana nchi zote duniani isipokuwa katika bara la Antarctica.

Kuna nchi ambazo zimefanikiwa kuuondoa ugonjwa huu kulingana na njia bora walizoweka na kuzitii za kupambana na ugonjwa huu.

Lakini kuna baadhi ya nchi hasa zinazoendelea (ikiwemo Tanzania) ugonjwa huu umendelea kujitokeza na kusababisha vifo kwa watu wake. Takwimu zinaonyesha kuwa watu kati 50,000 hadi 70,000 hufa kila mwaka duniani kote, hii si namba ndogo hasa tunapozunguzia uhai wa binadamu unaopaswa kulindwa kwa nguvu zote.

Ili ugonjwa huu usikuwepo Zanzibar, Ramadhani Juma Ramadhani ni msaidizai Daktari kitengo cha kudhibiti magonjwa kwa Wanyama ameshauri wananchi kupeleka hospitali Wanyama wao hususan Paka na Mbwa kupatiwa chanjo mapema na kwa binaadamu iwapo atatafunwa na mnyama asiyejua kama amechanjwa au laa afuate hatua hizi:

Akoshe kidonda kwa dakika 15 kwa kutumia sabuni na maji ya mtiririko baada ya hapo akimbilie hospitali kabla ya masaa 24 kupita.