Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Kati ya wagonjwa 13 waliothibitika na virusi vya CORONA nchini Tanzania ni mgonjwa 1 tu ambaye hakusafiri nje ya nchi

Kati ya wagonjwa hao 8 ni Watanzania na 5 ni Wageni. Arusha wapo wagonjwa 2, Dar es Salaam wagonjwa 8, Zanzibar 2 na Kagera 1 ambapo Wagonjwa 12 wote waliambukizwa nje ya nchi

Waziri amesema mgonjwa wa kwanza ameshapona virusi vya COVID19 na ataruhusuwa kurudi uraiani hivyo jamii isimnyanyapae, kumdhalilisha wala kumtukana

Aidha, amewashukuru watumishi wa afya wanaoendelea kuwatibu wagonjwa wanaobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya COVID19 na kuwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari ya Corona