Mabalozi wametakiwa kuendelea kuwaunga mkono viongozi wao katika kila hatua ili kupata maendeleo ya haraka

Hayo yamesemwa na mjumbe wa baraza kuu la taifa UVCCM ndugu Kassim Hassan Haji wakati wa zoezi la upachikaji wa bendera kwa mabalozi katika muendelezo wa magharibi ya kijani huko jimbo la mwanakwerekwe tawi la kidatu ambapo jumla la mashina 33 yameekwa bendera katika jimbo hilo.

mjumbe wa baraza kuu la taifa UVCCM ndugu Kassim Hassan Haji akizungumza na mabalozi

Amesema ushirikiano wao ndio uliofanya zoezi hilo kuwa jepesi na kuwataka mabalozi hao kuzitunza na kuhakikisha bendera hizo zinaendelea muda wote.

Aidha amesema lengo la kupachika bendera hizo ni kuwapa  uhai mabalozi hao katika kufanya kazi  zao na kuhamasisha wakati wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ifikapo 2020.

Kwa upande wake muakilishi wa viti maalum UVCCM Mh. Hamida Abdalla Issa  amewapongeza mabalozi na viongozi wa jimbo hilo kwa ushirikiano mzuri waliouonesha katika zoezi hilo na kuwataka endelee kufanya kazi kwa weledi.

muakilishi wa viti maalum UVCCM Mh. Hamida Abdalla Issa akipachika bendera

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake Bi Aziza Amour Hamis  ameahidi kuyafanyia kazi yale yote walishauriwa na viongozi wao.

Zoezi la upachikaji wa bendera kwa mabalozi katika muendelezo wa magharibi ya kijani limezinduliwa Novemba 28 mwaka huu na  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru   na linatarajiwa kumalizika Disemba 11 mwaka huu.