Usinyanyaswe: Zifahamu haki zako za msingi za kufanya pindi Askari akikuweka chini ya ulinzi

ZIFAHAMU HAKI ZAKO ZA MSINGI IMEANDALIWA NA MAWAKILI.

 1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
 2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukukamata, ni haki yako.
 3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
 4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kwa kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
 5. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
 6. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
 7. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kukuonesha kibali maalum cha kupekua ambacho hutakiwa kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
 8. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
 9. Usipekuliwa nyumbani bila kuwepo kiongozi wa mtaa.
 10. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi na kuhakikisha mali iliyochukuliwa lazima ibaki salama.
 11. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwanamke haruhusiwi kwa mwanaume.
 12. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
 13. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
 14. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
 15. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO.