Zaidi ya Bilioni 1 zatengwa kwa ajili ya matamasha ya Utalii Zanzibar

Zaidi ya Billioni moja zimetengwa kwa ajili ya matamasha ya Utalii zanzibar ili kutangaza vivutio vya utalii na historia ya Zanzibar.

Akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Ali Suleiman ali katika mkutano wa Baraza la wawakilishi chukwani Nnje kigodo ya mji wa Zanzibar.

Naibu Waziri wa Habari,Utalii na mambo ya kale Chumu Kombo amesema fedha hizo zitatumika katika mwaka wa fedha 2019/20 katika matamasha ya utalii yatakayosaidia kutangaza Rasilimali za kitalii zilizopo pamoja na kuimarisha mapato ya nchi.

Amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo watashirikiana katika kuandaa Onesho la utalii la Mwaka 2019 jambo ambalo litawapa fursa wafanya biashara kutangaza bidhaa zao.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendeleza mila na desturi za Mzanzibar ili kuwapa hamasa wageni kujifunza utamaduni uliopo.