Baada ya Marekani kuamuru vikosi vyake vya Kijeshi vilivyokuwa Syria mpakani mwa Uturuki viondoke, Uturuki imesema imekamilisha maandalizi ya mashambuli Kaskazini mwa Syria

Rais wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan ametishia mara kadhaa kuwashambulia Wanamgambo wa Kikurdi katika eneo hilo kutokana na uhusiano wao na watu wanaotaka kujitenga chini mwake

Awali, Rais Erdogan alisema mashambulizi hayo ya Kijeshi yanaweza kufanyika wakati wowote huku Wadau kadhaa wakisema shambulio lolote la Uturuki litasababisha mauaji ya halaiki ya Wakurdi

Aidha, Makamu wa Rais wa Uturuki, Fuat Oktay ameonya kuwa Taifa lake halitojibu mapigo kutokana na vitisho litashika njia yake na kushughulikia mambo yake yenyewe

Rais Trump alisema ni gharama kubwa kuendelea kuunga mkono vikosi vya Kijeshi vinavyoongozwa na kundi la Kikurdi katika eneo hilo katika kukabiliana na kundi linalojiita Dola ya Kiislamu