Mtu mmoja afariki katika ajali ya vespa kuugonga mti eneo la mlima Nguli ulipo Kiwengwa mkoa wa KaskaziniUnguja.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Unguja Mussa Ali Mussa amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na mbili jioni eneo la mlima wa Nguli.

Katika ajali hiyo vespa aliyokuwa amepanda marehemu haikupatikana na juhudi za kuitafuta zinaendelea.

Sambamba na hayo Kamanda Mussa amewataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu sheria za barabarani na kuacha kwenda mwendokasi.

Kamanda Mussa ameelezea chanzo cha ajali ni mwendo kasi aliokuwa akiendesha vespa hiyo hivyo imemshinda na kuugonga mti.

Rauhiya Mussa