Video: Meneja wa Diamond afunguka Uongozi wa WCB hukutana mara kwa mara na uongozi wa Alikiba

Mmoja kati ya mameneja watatu wa Diamond Platnumz, Sallam SK amedai kwamba viongozi wa WCB huwa wanakutana mara kwa mara na uongozi wa Alikiba na kuzungumza mambo mbalimbali.

Jumatano hii meneja huyo akiwa Times fm akifunguka mambo mengi huku WCB pamoja na muziki ambapo pia alifunguka kueleza kwamba sio kweli kwamba Diamond ana bifu na Alikiba huku akienda mbali zaidi kwa kudai viongozi wa label hizo mbili hukutana mara kwa mara.

“Kati ya Ali na Diamond hakunaga bifu, na haijawi kutokea, na uongozi wa Alikiba na WCB huwa unakutana mara kwa mara kuzungumza,” alisema Sallam. “Bifu ilitengenezwa na sisi baada ya kuona watu wanapenda hivyo vitu tukavitumia kwaajili ya kupromote wimbo wetu,”