Video: Mfahamu Dj Sam maarufu King of Philipiine mwenye kutafsiri Series za Philippine Zanzibar

Je ulishawahi kujiuliza DJ Sam maarufu KING OF PHILIPPINE  ni mtu wa aina gani?

Salum Abdalla Ali “DJ Sam” ni kijana anayejishuhulisha na kutafsiri Michezo ya lugha mbalimbali hususani ya Philippine kwa lugha ya Kiswahili.

Miongoni mwa michezo ya Philippine aliyotafsiri na ikapendwa sana ni Bagani, Twins Revenge, Ariana Galema, Dayosa n.k.

Zanzibar24 imefanikiwa kufanya mahojiano na Dj Sam ambaye ameeleza mengi kuhusiana na maisha yake ya kazi akiwa kama mtafsiri wa michezo na maisha yake.

Kupitia mahojiano hayo Dj Sam ameeleza kwanamna gani amefanikiwa kuwa msambazaji mkubwa wa filamu za Kiphilippino na watu wengi kukubali kazi zake hapa Zanzibar.

Uliwahi kujiuliza mtu huyu atakuwa na kiwango gani cha elimu? Angalia Video uweze kumsikia mwenyewe akijielezea.