Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda hapo jana usiku ameshusha maombi kwa vijana wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars waliopo Misri ili kufanikiwa kuifunga Kenya katika michuano ya Afcon2019.

’Tunamuomba mungu pasi zenu zikafike kwa walengwa, mkaonane Mungu akawape wepesi wa kufika kwenye magoli, akawe mlinzi wa goli letu na kila kinachowezekana ili kesho ikawe siku ya kutangaza utukufu wa Mungu mkubwa kwa ushindi wa Taifa Stars.’- RC Makonda