Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kitendo cha kupandishwa cheo kwa Askari wa Idara maalumu za SMZ  hakizingatii kigezo cha kumaliza kozi kwa askari wa Vikosi hivyo.

Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Naibu Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na
Idara Maalumu za SMZ Shamata shame Khamis amesema  upandishwaji wa Cheo kwa Askari unatokana wa Umahiri katika kutekeleza Majukumu yao.

 Amesema pia kupandishwa cheo kwa Askari kunatokana na Mahitaji ya kimuundo kwa kikosi husika ,Bajeti ya kikosi ,Mahitaji maalumu ya kikosi  pamoja na Askari kufaulu kozi anazopitia.

Alisema kupandishwa cheo ni hatua muhimu ya kumuendeleza mtumishi na kumpa motisha katika utendaji kazi wake.

Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 22(1) cha sheria ya utumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 2011 Afisa wa Idara Maalumu za SMZ anaweza kuongezewa muda wa utumishi usiozidi miaka miwili endapo itaonekana ipo haja ya kufanya hivyo kwa lengo la kutoa ujuzi zaidi.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.