Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi amewapongeza vijana kwa juhudi walizochukua za  kupinga  udhalilishaji na mapenzi ya  jinsia moja jambo ambalo linapoteza nguvu kazi ya Taifa .

Ameyasema hayo wakati wa Mapokezi ya Maandamano kwa  vijana wazalendo wa Zanzibar wanaopinga ushoga na udhalilishaji  huko Ofisini kwake Mazizini.

Alisema amewapongeza vijana hao kwa juhudi waliyoichukua kwa kupiga vita ushoga na udhalilishaji katika hali ya amani na utulivu nchini.

“Mfumo wetu wa maisha unapinga vitendo vya udhalilishaji na kuoana jinsia moja wala hautaki ubaguzi wa rangi dini wala kabila “ alisema Mufti .

Aliwataka vijana kuachana na wigo wa tamaduni za kigeni ambao unaharibu nguvu kazi wa taifa.waendelee kulinda miongozo ya Dini  pamoja na mila Silka na tamaduni za asili.

 Aidha aliwaahidi vijana kushirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha vitendo hivyo vinaondoka nchini na watu wanaishi katika maisha ya kuridhiwa na Mwenyezi Mungu duniani na akhera .

Nae Kijana Mzalendo Khamis Rashid Kheir (Makoti) alisema suala la ushoga na udhalilishaji kwa wanawake na watoto hatutolivumilia tena katika nchi yetu .

“Tumeshachokaa tena ndugu zetu kufanyiwa vitendo vya ushoga na udhalilishaji ni kinyume na mila desturi na tamaduni zetu katika dini zote mbili si za kiislamu wala kristo hazihitaji vitendo hivyo , “ alisema Makoti .

Alieleza iwapo vitendo hivyo vinachangiwa na viongozi au mtu wa kawaida Vijana wameamua kuondoa sera za kishoga katika nchi yao.

Nae Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar Mohamed Said Abdalla  amesema  vijana wazalendo wanapaza sauti zao ili kupinga kadhia hiyo ikiwemo ushoga na udhalilishaji pamoja vitendo vyote anavyopinga amri ya Mwenyezi Mungu ambavyo sio halali kuvifanya.

Amesema wanaiomba Serikali ijayo ya awamu ya nane   kutolifumbia macho suala hili kwani hata viongozi waliokuwemo madarakani wamelipinga vikali suala hilo lakini bado linaendelea siku hadi siku jambo ambalo linaathiri vijana kimaendeleo.