Vijana  nchni wametakiwa  kubuni mbinu  za kujiajiri wenyewe zitakazowasaidia katika kujikwamua na tatizo la ajira ambalo limekuwa ni kilio kikubwa kwa taifa hasa kwa vijana wasomi waliomaliza  elimu yao ya juu.

Akizungumza na Zanzibar24  Mmoja wa kijana  Saleh Salum Saleh aliyeweza kujiajiri wenyewe zaidi ya miaka kumi kwa kazi ya ujasiriamali  ya kutengeneza bidhaa zinazotokana na mabati  amesema kutokana na uhaba wa ajira kutoka serikali vijana hawana budi kutafuta njia mbadala  itakayowasaidia kujikwamua  na tatizo hilo la ajira ili kuweza kupata kipato.

Amesema kuna  fursa  nyingi  za kufanya katika shughuli za ujasiriamali  na endapo  vijana   wakiwa tayari  kuzitumia vyema fursa hizo  tatizo la ajira litaondoka nchni na itaiyondoshea serikali mzigo wa utegemezi.

Aidha Saleh amesema tokea kuanza kazi hiyo ya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutumia mabati na vyuma ameweza kufaidika kwani kwa siku amekuwa ikiingiza zaidi ya laki moja,kusomeshea watoto wake pamoja na fedha hizo kutumika kwa mahitaji mbalimbali katika familia yake bila ya kumtegemea mtu au serikali.

Ambapo ametoa wito kwa serikali kuzidisha juhudi za kuwaelimisha  vijana kujiajiri  wenyewe kwani bado fursa zipo za ubunifu.

Amina Omar