Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya linawashikilia vijana Watano kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma na mshale shingoni mwalimu Justine Sospeter Ogo wa shule ya sekondari Itiryo.

Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya Henry Mwaibambe alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya Asubuhi Novemba 14,2019 Katika kijiji cha Itiryo.

“Chanzo cha mauaji hayo ni vijana hao wapatao wanane wakiwa wanatembea Barabarani wakiwa na silaha za jadi wakiwa wanajiandaa kwenda kwenye Tohara mwezi wa 12 mwaka huu walikuwa wanasimamisha watu na kuwaomba Fedha kwa nguvu kuonyesha ujasiri,ndipo Marehemu alikuwa anampeleka mwalimu mwenzake kusimamia mitihani ya kidato cha Nnee inayoendelea katika shule ya Sekondari Bungurere wakamsimamisha na kuanza kumdai awape fedha mwalimu na wenzake wakawa wanaondoka bila kusimama ndipo kijana mmoja wapo alimchoma na mshale shingoni kutoka upande wa kulia  na kutokea upande wa kushoto alifariki alipofikishwa Hospitali,”alisema Mwaibambe.

Mwaibambe aliongeza kuwa vijana watano wamekamatwa kati ya vijana wanane wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na Jeshi la polisi linaendelea kuwasaka vijana wengine waliobaki ili kuwakamata na kuwapeleka sehemu husika.

Mwaibambe alisema umri wa vijana hao unachunguzwa wakati alipokuwa akitaja majina ya vijana hao kuwa ni pamoja na Nchore Richard,Marwa Mwita Gichome,Gisiri Simion Mhere,Makenge Hongo Chacha na Muhere Mwita Gichumu na kuwa wanaoshikiliwa huku wakihojiwa na hatua zikikamilika wanahojiwa ili hatua za kuwahoji zikikamilika watafikishwa sehemu husika kuwa ni pamoja na na kuwa uri wa hao vijana unchanguzwa.

Kamanda huyo ametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi,walezi na wananchi kwa ujumla kuwafunza watoto wao maadilimema kwa jamii vinginevyo sheria haitasita kuwachukulia hatua kali watoto wote wsanaojihusha na vitendo vyovyote vya kihalifu.

Awali akisimulia tukio hilo mwalimu Nicku Shamukoma Bariki wa somo la Taaluma shule ya Sekondari Itiryo alisema kuwa mwalimu huyo aliuawa akiendesha pikipiki wakati akiwa njiani na wenzake wawili aliokuwa amewapakia huku wakielekea  Shule ya sekondari  Bungurere ili kusimamia mitihani ya Kidato cha Pili na Nne inayoendelea.