Wananchi wa Mkoa Wa Kaskazin Unguja wametakiwa kutoa ushirikiano na jeshi la polisi ili kukabiliana na makosa mbali mbali Ya uhalifu pindi pale yanapotokea na kuwataka kutoa taarifa hizo za Uhalifu iliziweze kufanyiwa kazi.

Kauli hiyo ameitoa Kamanda Polisi Mkoa wa Kaskazin Ungujaa Haji Abdallah Haji kupitia tukio la kukamatwa kwa vijana wawili wakiwa na kete za Heroine 1,428 zinazosadikiwa kuwa dawa za kulevya zenye Uzito 64.26 grams huko Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Kamanda Haji amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Imrani Ameir Yussuf mwenye umri wa miaka 35 mshirazi wa Mtoni Kidatu Wilaya ya Magharibi  A pamoja na Hassan Kassim Yussuf mwenye umri wa miaka 20 mshirazi wa Chumbuni wote kwa pamoja wamekamatwa wakiwa na kete za heroine katika gari yao yenye usajili no. Z. 842FE iliyotoka mjini kuja Nungwi.

Watuhumiwa wote hao wapo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi pamoja na gari yao utaratibu utakapokamilika katika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

Kamanda Haji ametoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya na kuwataka kutambua kuwa yoyote atakae kamatwa na dawa za Kulevya katika magari au katika majumba basi watambue kuwa ipo sheria ya dawa za Kulevya kustaafisha mali hizo kupitia mahakama .

Rauhiya Mussa Shaaban