Jumla ya vilabu  kumi na Tano vinatarajia kushiriki kwenye mashindano ya kutafuta  klabu Bingwa wa  Riadha Zanzibar mwaka 2018/2019. itakayofanyika mwezi wa Septemba mwaka huu kwenye uwanja wa Aman Mjini Unguja.

Akizugumza na zanzibar 24 Katibu wa chama cha Riadha Zanzibar Sleman Ame  Nyambui  huko ofisi ya kuu ya chama hicho eneo la uwanja wa Amani mjini Unguja alisema wao kama cha Riadha kwenye kalenda ya mwaka mzima wanatarajia kuwa na mashindano hayo kwa wanawake na wanaume kwa timu zote za Unguja na Pemba.

Aidha alisema kuhusu mandalizi ya mashindano ya kutafuta klabu Bingwa amesema tayari wameshafata taratibu walizopewa na Baraza la Michezo Zanzibar kwa kuhakikisha vilabu vinavyoshiriki mashindano hayo vimesajiliwa na BMTZ na kukamilisha taratibu za katiba zao.

Kwa upande mwengine Nyambui alisema Bingwa wa mwaka 2017 atatea ubingwa wake mwaka huu mwaka 2018 ambae ni klabu ya KMKM,kwa upande wa kuongezeka klabu mpya mpaka sasa na tayari wameshapeleka barua kwa vilabu vyote na kutakiwa kulipa ada kwa vilabu vyote washiriki.

“Vilabu vyote kumi na tano vinatakiwa kulipa ada na kuambatanisha majina ya wachezaji wao watakaoshiriki na watanikiwa wachezaji wa nane tu watakaoshiriki mashindano ya mbio na kurusha na mbio fupi  kamati ya ufundi ndio itakae simamia utaratibu wa kujiunga”Alisema Nyambui.

Kwa upande wa wa dhamini Nyambui amesema tayari BMTZ ndio wadhamini wao wa kwanza na wakubwa kwa kutengewa fungu maalum na wapo wadau wengi wako tayari kuwasaidia na bado wanakaribisha wengine kuwasidia .

“Idara ya elimu,utamaduni na michezo inatarajia kuleta vilabu vyake vya watoto vya Sports 55 ili kuweza kuibua vipaji vya watoto japo tumewandalia mashindano yao maalum kwenye kalenda yetu ya mwaka huu “ Alifafanua Nyambui.

Mashindano ya Riadha kutafuta klabu Bingwa Zanzibar yanatarajia kuanza Septemba mosi hadi pili ili kutafuta Bingwa wa Zanzibar kuwakilisha kwenye mashindano ya Afrika Mashariki na kati wakati Bingwa mtetezi ni Klabu ya KMKM kwa mashindano yote ya jumla.