Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa imewatahadharisha Wafuasi wa Vyama vya siasa vilivyopo Nchini kuacha tabia ya kutumia mihadhara ya dini kwa kuhubiri siasa zao.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Muhamed Ali Ahmed wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Katika ukumbi wa Ofisi hiyo Bweni Wilaya ya Magharibi b Ungujaa.

Amesema kuna baadhi ya wafuasi wa Vyama vya siasa wamekuwa wakiitumia vibaya dini kwa kuishirikisha na suala la siasa jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Amesema kufanya hivyo ni kukiukaa Sheria na taratibu za  Usajili wa Vyama vya siasa jambo ambalo litasababisha matabaka kwa waumini wa dini mbalimbali.

 ’’Si suala la busara kuona wanachama wanachanganya  dini na siasa ,kufanya hivyo ni kosa na Ofisi yetu haitakivumilia chama chochote hata kama kikubwa na kina wafuasi wengi badala yake tutakichukulia sheria’’ ..Alisema Naibu huyo

Amesema katika kuhakikisha sheria na taratibu za siasa zinafuatwa nchini Ofisi hiyo haitamvumilia mtu yoyote atakaekiuka amizo hilo ili kuimarisha amani iliopo.

Hata hivyo amewataka viongozi wa dini kutumia nafasi walizonazo katika kukemea waumini wao kutochanganya siasa na dini ili kuendeleza heshima na taratibu za dini zao.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24

fathiyashehe@gmail.com