Vipi unaweza kumkinga mwanao na utapia mlo?

Mpangilio mzuri wa ulaji wa vyakula bora humjenga mtu kuwa na afya bora ya kimwili ,kiakili pia kuwa na mfumo mzuri wa ukuaji na kuufanya mwili kuwa na lishe bora ambayo ndio kinga ya mwili na maradhi mbali mbali pia msingi wa maendeleo wa maisha ya sasa na baadae .

kawaida mwanaadamu anatakiwa kula mlo kamili wenye mchanganyiko wa virutubisho mbali mbali kama vile  protini ,vyakula vyenye uwanga ,mafuta halisi ,vyakula vya vitamini (mbogamboga na matunda) na vyakula vya madini (mineral) ambavyo huufanya mwili kuwa na lishe ya kutosha na uimara katika maisha ya kila siku kwa sababu lishe bora huulinda mwili na maradhi mbali mbali.

Kumbuka kuwa mtu ni afya na afya ni  lishe bora ,inapokosekana yakutosha katika mwili hufanya mwili uweze kushambuliwa na vijidudu vya maradhi  kwa urahisi na hata mwili kuwa dhaifu na kupatwa  maradhi mengi ikiwemo utapiamlo, ambao ni hatari kwa kwa maisha ya watu wa rika zote (watu wazima na watoto) hususan  kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa afya kutoka wodi ya watoto katika hospitali ya Mnazi mmoja daktari Hadiya  Mahadhi Haji ameelezea kuwa ‘Utapiamlo ni hali inayotokana na unyonyeshaji na ulishaji usio sahihi ambao  unaweza kufanya mwili kuwa na lishe duni na hatimae kupata maradhi .

Ameeleza kuwa maradhi haya ni moja kati ya matatizo muhimu ya kiafya Zanzibar haswa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na thuluthi ya vifo vya watoto wa umri huo husababishwa na utapiamlo mkali na husababisha vifo vya watoto kwa asilimia hamsini (50%).

Dk Hadiya Mahadhi Haji ameeleza kwamba Maradhi haya ya utapiamlo yapo ya aina tafauti, ambayo ni; Utapiamlo wa  ukondefu (wasted) hali hii hutokea kwa muda mfupi ambapo mtoto hupungua uzito sana kulinganisha na kimo/urefu alionao .

Pia amefahamisha Utapiamlo wa muda mrefu yaani  udumavu (stunted) huu mtoto huwa na urefu /kimo pungufu kulinganisha na umri  alionao.

Uzito pungufu(underweight)ni moja ya aina za utapia mlo mtoto kupungua uzito ambao hauwendani naumri alionao.

Ukosefu wa virutubisho yaani mtoto kukosa vitameni na madini kwa mfano madini yachuma(iron), madinijoto(iodine) , navitameni ,Uzito mkubwa kwa kimo (over weight/obesity) yaani kua na uzito kupitiliza ambao hawendani na kimo alonacho.

Dk Hadiya Mahadhi ameeleza sababu nyingi zinazo sababisha kukithiri kwa maradhi ya utapia mlo mtoto endapo akikumbana nazo kwanjia moja au nyengine huwa ni dalili ya kupata maradhi hayo.

Kukosa chakula bora ni miongoni mwa sababu za watoto kupata maradhi haya hii inaweza kusababishwa na umaskini ,kukosa elimu au mila potofuwengine wamekosa elimu ya lishe na kushindwa kuwalisha chakula vizuri na hatimae  kusababisha utapiamlo.

Aidha dk Hadiya Mahadhi ameeleza miongoni mwa sababu nyengine ni Kutowatunza vizuri watoto na mamahii hususa ni kwa akina baba ambao wanashindwa kuwahudumia vizuri mama mzazi ili aweze kumlisha mtoto kwa ubora na wengine wanawatelekeza wamama na  watoto wachanga na kushindwa kujihudumia yeye na mtoto wake na kumfanya kukutwa na lishe duni na hatimae hupata utapiamlo.

Kukosa huduma bora za kiafya wapo baadhi ya wazazi na walezi hawafuatilii masuala ya chanjo za watoto na jinsi ya kutumia dawa kwa watoto kitu ambacho kinamfanya mtoto kupoteza afya yake na kumsababishia utapiamlo.

Mazingira hatarishi kwa watoto ; kuna akina mama wazazi ambao hawawa shughulikii vizuri watoto na kujiingiza katika mazigira machafu kama makaro ,kuchezea matakata machafu na kuyatia mdomoni na kusababishia hali ya kiafya kua mbaya na kukumbwa na utapiamlo.

 Maradhi ;uwepo wa magonjwa yenye kudhoofisha kinga za mwili kuna changia kuwepo kwa utapiamlo kama vile Tb,kisukari ,Hiv ,homa ya taifodi,na magonjwa sugu kama vile  ungonjwa wa moyo hususa kwa watoto.

 Mabadiliko ya tabia ya nchi ; pia kubadilika kwa mionga ya mwaka na mazingira kua tofauti inafaya uzalishaji wa vyakula kupungua na kushindwa nikutumia vyakula vizuri na kutumia vyakula vya kemikali nihatari kwa afya zetu na watoto na kumfaya kupata utapiamlo.

Machafuko ya hali ya  kisiasa nchi ; hali humtia mzazi hofu na kushindwa kumuhudumia mtoto vizuri kwa kuwa na mawazo ya machafuko na kukimbilia mafichoni ambako hali ya uchumi ni hafifu sana na kumfanya mtoto kuapata utapiamloa kwa mfano Somalia .

Tunahiataji unagalifu mkubwa katika kuhakikisha tunaepuka sababu za maradhi haya yautapia mlo katika jamii yetu ambayo ni wathirika wakubwa Dk Hadiya Mahadhi aneeleza dalili za maradhi ya utapia mlo ambazo ni ni rahisi kuzigundua.

Amelezea kuwa maradhi haya yana dalili na ishara nyingi ambazo zinajulisha mtoto kuwa amesha patwa na utapiamlo na nyengine ningumu kutambua mpaka imuathiri sana na  dalili pamoja ishara hizo zipo za ukondefu na hali ya kawaida (kwashiakor).

Dalili za Zaukondefu .

Kupungua uzito sana na kukonda ;mtoto kukonda  na ngozi kukunjana  kama mzee na uzito hupungua kwa kiasi kikubwa sana.

Kutokeza kwa mifupa ya mbavu ; mifupa ya mbavu kijitokeza na kuiyona kama isiyo na nyama ipo na ngozi tu .

Mikono na miguu kua membamba sana .

Mzunguko wa katikati ya mikono ya juu (MUAC)kuwa chni ya 11.5 cm.

Kupungua misuli sana .

Nywele kua kama sufi na kubadilika rangi .

Kuongeza hamu ya kula /kula sana mpaka hajui saizi yake .

Kufanya kitumbo ambacho hakiendani na alivyo.

Kujitokeza kwa mifupa ya mabega .

 Mtoto mwenye dalili na ishara hizi yapo  matokeo mazuri akipatiwa matibabu mazuri.

Kikwashiorkor/muonekano wa kawaida.

Kuvimba na kubonyea kwa miguu yote miwili .

Kuvimba uso ,mikono na tumbo.

Nywele kuwa nyepesi na rahisi kukatika na kugeuka rangi nyekundu.

Kukosa hamu ya kula.

Kuwa mkali na kuchukia watu.

Kufanya vidonda mwilini.

Mtoto mwenye dalili na ishara hizi yupo hatarini na uwezekano mkubwa wa kufa.

Mtaalamu Dk Hadia imeweka bayana athari za maradhi ya utapia mlo ambazo kama watoto zitawakuta ni hatari katika familia na ngazi ya jamii kwa ujumla.

Maambukizi ya mara kwa mara ;kutokana na kutokuwepo kwalishe bora mwilini humfanya mtoto mwenye maradhi ya utapimlo kuweza kupata maambukizo ya maradhi mengine kwa sababu mwili bila lishe hauna kinga na bila kinga vijidudu vya maradhi huchambulia kila mara.

Kudumaa kiakili ;mtoto anapo athiriwa na utapiamlo akili yake huwa haipo vizuri na hatimae kukosa wataalamu ,nguvu kazi katika taifa .

Kukosa kujiamini na kutokushiriki katika shughuli mbali mbali maendeleo na michezo ;  hii nikwasababu utapiamlo humuasiri mtoto mfumomzima wa akili na kumfanya ushirikiano mzuri na wenzake kwa michozo na kua na wega .

Kuongeza mzigo wa matatizo kwa familia na jamii pamoja na taifa kwa jumla ; kutokana na kuathiriwa na utapiamlo mama au mlezi au familia inashindwa kufanya kazi kwa ufasaha na kukushulikia wewe upate huduma za kila kitu kwani inakua hauna nguvu za kujihudumia.

Kusababisha magonjwa ya moyo ,sindkizo la damu na kisukari.

Kuongezeka kwa maradhi na vifo katika taifa ;hivokukosa rasilimali watu ambao ndio taifa la kesho na maendeleo ya baadae  .

Doctari Hadia amesisitiza kuwa Maradhi haya ya utapiamlo nimaradhi yanayo tibika kwa uraisi japokuwa nihatari kwa watoto na yapo matibabu ya   kitaalam ( Hospitalini) na ya kawaid   endapo  mgonjwa atafata utaratibu wa madaktari na kuhudhuri katika chanjo za watoto na vituo vya afya .

Kwa upande wa matibabu ya hospitali Dk Hadia ameeleza  kuwa Maziwa maalumu kwa utapiamlo (F-75 na F 100)ambayo hupatikana hospitali nakupewa watoto ili weze kuwa na lishe ya kutosha katka mwili na kumfanya awe katka afya mzuri,( Ready to use therapeutic food (RUTF  ).       

Madawa ya hospitali ni miongoni mwa matibabu  yapo madawa maalumu haya ni maalumu kwa watoto wenye utapiamlo ambayo humtibu mtoto kwa haraka na kuwa na afya bora.

Dhana ya kuwa maradhi ya utapia mlo hayatibiwi nyumabani dk Hadiya hapa aneeleza jinsi unavyoweza kutibu maradhi haya kwa njia za majumbani.

Unyonyeshaji wa ziwa la mama ni miongoni mwa matibabu ambayo dk Hadia anayatilia mkazo sana  “kumpatia mtoto maziwa ya mama ambayo yana mkusanyiko wa nyakula vingi ndani yake na  bila ya kumpa chakula chengine kama hajafikia miezi sita  isipokua dawa ulizo shauriwa na daktari au muuguzi” alitilia mkazo Mtaalam huyo wa Afya.

“Afya ni Cha kula” Mlo kamili ni kinga tosha na matibabu ya kujikinga na maradhi haya ya utapia mlo dk Hadia aneeleza kuwa kumpa chakula chakutosha mototo au mgonjwa na chenye lishe yaani virutubisho vyote pale anapofikia miezi sita ambapo unaaza kumlisha chakula kwa utaratibu mzuri.

Wizara ya Afya kupitia kitengo chake cha watoto wanafanya juhudi mbali mbali ili kuhakikisha wanapambana na maradhi ya utapia mlo mbapo kimsingi jamii imesahau kuhusu maradhi haya na wanatombinu zinazotumika kupambana na maradhi haya.

  Mingoni nazo ni Kuwafunza wanajamii juu ya elimu ya maisha na uzalishaji mali, Kutilia nguvu juu ya matumizi ya vituo vya afya na kuacha kujitibu majumbani kwa kutumia madawa asili pasipo na utaalamu, Kutaka ushauri wa madaktari mapema mara tu unapoona mabadiliko mabaya ya ukuaji wa mtoto

Kuwachunguza watoto dalili za utapiamlo katika jamii zetu kila fursa inapojitokeza.

;kwa mfano

Kuwafuata watoto na kuwachunguza mashuleni ,vijijini na mitaani.

Kampeni za chanjo , utoaji wa madawa za minyoo na vitameni A.

Mikutano ya kijamii katika makundi ya kina mama.

Kutembelea majumbani.

Nae mkasi khamis Ali (45) mkaazi wa kwarara   ameelezea kua maradhi haya ya utapiamlo ni kunyonyesha kidogo kwa wamama.

Amesema yeye mtoto wake amepata utapiamlo kwa kua alikua akinyonyesha mtoto kwauchache haliambayo ilimfanya kudhoifika kiafya na kugundua ni unyonyeshaji mbaya .

“Mwazoni nilikuwa sina elimu ya utapiamlo kwani nimpeleka mtoto hospitali kwa kumuona ni homa na baada ya kupata vipimo alimbiwa ni utapia mlo” alihadithia mama huyo.

Hatahivyo mama huyo ametoa ushauri kwa wazazi kwa kuwashughulikia watoto na kuwanyonyesha maziwa ya mama pekee miezi 6 ya mwanzo bila kumpa hata maji isipokua dawa kwa ushauri wa daktari.

Vilevile amewataka wababa wawe na mashirikiano mazuri kuwashughulikia watoto pamoja na kuwapa vyakula vizuri wamama wajauzito ili anapomzaa mtoto awe na afya mzuri na mama kuwa na maziwa ya kutosha ambayo ndio kula ya mtoto miezi 6 ya mwanzo.

 Mosi Muhammad Bakar mkazi wa Bubwini (23) ambae ana mtoto muathirika wa utapiamlo ameleza kuwa ufahamu wake utapia mlo ni kukosa virutubisho mwilini ambavyo vinatokana na maziwa ya mama pamoja na vyakula bora.

Aliendelea kusema mwanzoni alikua hana uwelewa mzuri kuhusu maradhi ya utapia mlo na amemleta mtoto hospitali ya Mnazi Mmoja kwa homa ila akaambiwa ni utapia mlo hivyo amepewa matibabu na elimu juu ya maradhi hayo na kuelewa vizuri na jinsi ya kunyonyesha na kumpa chakula mbacho ni stahiki pale anapofikia miezi 6 pamoja na kuendelea  kumyonyesha mpaka miaka 2.

Kwa mujibu wa kitengo cha lishe  Zanzibar, maradhi ya utapiamlo kwa mikoa ya Zanzibar  takwimu zinaonyesha kua mwaka 2017.

Utapiamlo wa udumavu kwa Zanzibar nzima ni 24% na mkoa unaongoza kwa utapiamlo  ni kaskazini pemba kwa 34% ,ikifuatiwa na kusini unguja 27%,  kusini pemba 24%,   kaskazini unguja 23% ,na  mjini magharibi 17%.

Na kwa utapiamlo wa ukondefu kwa Zanzibar nzima ni  7%  na mkoa unaongoza ni kaskazini pemba kwa 9%,  kusini pemba 9%,  kusini unguja 8% , kaskazini unguja ni 6%,  na mjini magharibi 5%.

Pia kwa utapiamlo wa uzito pungufukwa Zanzibar nzima ni 14% na mkoa unaongoza kwa utapiamlo huu ni kusini unguja kwa 18%,   kaskazini pemba 17% ,  kaskazini unguja na kusini pemba 14%, na mjini magharibi ni 11%.

Makadirio  ya watoto chini ya miaka mitano  wenye utapiamlo mkali  kiwilaya kwa wilaya zote Zanzibar  ni kama ifuatavyo:-

Wilaya ya Magharibi  ni watoto    1572  , Mjini 1000 , Kaskazini A 508 ,Wete 462 ,Micheweni 444 ,Mkoani 404 ,Chake 402 ,Kaskazini B 385 ,Kati 146 na Kusini 64 .

Kwa jumla ni watoto 5387 ambao wanakadiriwa kupatwa na tatizo la utapiamlo mkali sana ,idadi hii kubwa sana inaonesha kuwa utapiamlo bado ni changamoto kubwa katika jamii ya kizanzibari.

Hivyo hatunabudi kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu wakiafya na watoa elimu juu ya lishe bora kwa watoto najinsi ya kuwanyonyesha watoto kwa kumpa maziwa ya mama pekee na kuachana na imani za kishirikina.

Na: Ibrahim Makame.