Viungo waliong’ara na kulitendea haki duara la kati (Maestro Midlfied Zanzibar)

Zanzibar ni lulu ya maendeleo ya maendeleo ya vipaji vya soka na kwa muda mrefu Zanzibar imekuwa ikizalisha vijana wenye uwezo wa kucheza mpira wa miguu na kuuchezea mpira wanavyotaka kwa lugha ya sasa tunawaita mafundi wa kuuchezea mpira .

Tumepita kwenye vipindi tofauti vya mafanikio ya mpira wa miguu Zanzibar na mafanikio makubwa yalikuwa yakiletwa na wakufunzi wa waliobobea kwenye fani ya mpira wa miguu ,licha ya Zanzibar kutotambuliwa na shirikisho la mpira duniani FIFA ila imekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya mpira wa Tanzania.

Msomaji wa makala hii yetu leo ntakuonyesha nyota wa Zanzibar walikuwa wakicheza nafasi ya kiungo (Mid field) kwa miaka ya zamani sana ambao ndio zao la wachezaji wa sasa kina Feisal Salum, Mohamed Issa Banka, Ibrahim Rajabu (Jeba),Hamadi Mshamata,Abdulswamad Kassm (GUTI),Mudathir Yahya Abas na wengine wengi waliopata mafanikio kwenye kizazi cha sasa.

Kwenye miaka ya kuanzia 80 zanzibar imekuwa ikisifika na wachezaji wengi wenye uwezo wa kuuchezea mpira mkubwa sana (Maestro) katika vilabu vya hapa hapa nyumbani Zanzibar wakati huo kulikuwa na ligi kuu ya muungano kutafuta Bingwa wa muungano (Super league).

Yako majina mengi sana haya ni baadhi ya tu ya machache ambayo ukiyataja lazima yakumbukwe kwenye ramani ya mpira wa Afrika mashariki na kati kwa ujumla , kwa juhudi zao walizozionyesha wakiwa uwanjani na mchango wao mkubwa kwenye mpira wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Saidi Ibrahim Junju, moja ya majina makubwa sana waliosifika kwa kuuchezea mpira wanapokuwa kiwanjani miaka ya thamanini ,wakati akiwa anachezea klabu ya Miembeni Sports Club nafasi ya kiungo .

Pia aliwahi kuchrezea timu ya Taifa ya Zanzibar na Timu ya Taifa ya Tanzania kwa miaka hiyo kwa mafanikio makubwa.

Kwa sasa ni mstaafu shirika la umeme Zanzibar anaendelea na shughuli zake za kawaida .

Ali Sharifu Adofu, moja ya viungo hatari waliowahi kungara visiwani Zanzibar na majina ya kusifika mitaani hadi sasa jina lake halijafa kwenye masuala ya mpira wa Zanzibar kwa sasa.

Mchezaji wa Al Noor mwaka 1885-1886 , na kujiunga na klabu ya Malindi kwa muda mrefu na kumalizia mwaka 1997 baada ya klabu hiyo kupoteza muelekeo alikuwa kiungo mzuri na kupata sifa kubwa visiwani zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Kwa sasa Adofu ni mwenyekiti wa soka la ufekweni Zanzibar ,pia ni kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya soka la ufekweni Zanzibar na amepata mafanikio makubwa kwenye soka la ufekweni Zanzibar baada ya Sand Heros kuchukua ubingwa wa mashindano ya Copa Dar Es saalam Beach Soccer.

Sheha Khamis (kaptein Sheha), moja ya majina maarufu kwenye mpira wa Zanzibar kwa wale waliowahi kumuona wakati akilitumia vilivyo eneo la kiungo ,hakua mchoyo wa kwa kutoa pasi na aliweza kusifika miaka ya 80 tangu akiwa kijana.

Alipata nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya Zanzibar mwaka 1995 na kuleta mafanikio makubwa baada ya kuchukua ubingwa wa CECAFA na akiwa nahodha wa timu hiyo ya Zanzibar Heros dhidi ya Uganda.

Kwa sasa ni amebaki kwenye maisha ya mpira wa Zanzibar ni mkufunzi wa leseni B ya aliwahi kuifundisha Taifa ya Jangombe na kwa sasa ni mkufunzi wa timu ya KVZ inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar .

Omar Kombo Msomali, yeye ni mchezaji wa KMKM wakati wa miaka ya 1980 wakati huo KMKM ni Bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar na kuwakilisha kwenye ligi ya Muungano .

Alichezea nafasi ya kiungo na aliwahi kubahatika kuuchezea timu ya Taifa ya Zanzibar 1892 kwa sasa ni mkaazi wa kisiwani Pemba na shughuli zake za kawaida.

Khamisi Mpemba, aliwahi kungara kwenye klabu yake ya Small Simba  mwaka 1992-1993.

Kwa sasa maisha yake yapo nje ya nchi nchini Uingreza.

Abdul Wakat Juma
Abdul Wakat Juma

Abdul Wakat Juma, jina kubwa sana hili kwenye maisha ya mpira wa Zanzibar, sisi vijana wengi wa sasa hatumjui kwa kile alichokuwa akikifanya akiwa uwanjani hususan eneo la kiungo mchezeshaji ambalo alikuwa akilitendea haki kiukweli.

Mwaka 1980-1990 alikuwa akitumikia klabu yake ya Small Simba .

Aliondoka kuelekea uarabuni kwenda kuchezea klabu ya Fanja na alibahatika kucheza timu zote za Taifa sasa hivi yupo anaendelea na shughuli zake za maisha za kawaida visiwani Zanzibar.

Makame Haji, mchezaji wa Muembe ladu ,Small Simba mwaka 1980 aliweza kulifanyia kazi duara la kati kama kiungo mchezeshaji.

Aliwahi na kubahatika kucheza timu zote za Taifa kwa Upande wa Zanzibar na Tanzania.

Nassor Moyo, moja ya majina ya kizazi cha mpira kwa muda huo wakati wa miaka ya thamanini na ilifanya kuwa kinara klabu ya Kikwajuni kwa kuweza kulitumikia duara la kati sehemu ya kiungo .

Pia mungu amempa bahati watoto wake leo wamerisi kipaji cha Baba yao ni baba wa familia ya mpira wa miguu Zanzibar kwa sasa watoto wake Hassan Nassor (Abal) ni mchezaji wa klabu ya Ndanda ya inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara kabla ya hapo alikuwa akitumikia Villa United na moja kiungo wa klabu ya Kvz ya ligi kuu ya Zanzibar Mohamed Nassor (Jaba) kabla ya hapo alitumikia klabu ya Kijichi pia ni mchezaji wa Zanzibar University.

Omar Hassan King, moja ya majina makubwa wakati wa 1986-96, lilikuwa jina kubwa wakati akiwa uwanjani jinsi alivyokuwa akiutendea haki mpira wakati akiwa klabu yake ya Small Simba chini ya mkufunzi kocha Musoma.

Kwa sasa ni mtumishi wa uma wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, nafasi ya katibu mkuu wa wazira ya vijana,sanaa na michezo chini ya wizara ya michezo.

Mcha Khamisi (marehemu), moja ya viungo walikuwa walipata sifa kubwa wakati huo wa henzi zao miaka 80 katika klabu ya KMKM wakati huo alikuwa bingwa wa Zanzibar kuwakilisha ligi ya muungano.

Ni Baba wa mchezaji wa mahiri Khamisi Mcha ambaye amecheza klabu ya Mafunzo,Azam na sasa anatumikia klabu ya Ruvu Shoting .

Yeye na mwanawe wote wamebahatika kuzichezea timu za Taifa ya Zanzibar na Tanzania.

“Mungu amrehemu amjalie maisha mema ya kaburini na kesho Akhera “Amiin.

Nassor Mwinyi Bwanga, aliwahi kuuchezea timu za Black Fighter,Malindi miaka ya 1986 kwenye ligi kuu ya Zanzibar kwa mafanikio makubwa sana sehemu ya kiungo .

Pia ni mchezaji aliepata bahati ya kucheza timu zote za Taifa Taifa ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa moja ya wachezaji waliojipatia nafasi kubwa kwenye soka la zanzibar .

Yako majina mengi ambayo yalikuwa yanatumia vizuri eneo la kiungo ni dalili za wazi Zanzibar ni nchi inayozalisha wachezaji viungo (Maestro),majina kama vile Karume Mussa alicheza Small Simba 1980 na kucheza timu zote Za Taifa na ile ya Zanzibar mwaka 1985.

Kina Omar Maneno klabu ya jamuhuri 1985 wakati huo jamuhuri ni Bingwa wa ligi ya Zanzibar ,khamisi Pele ujamaa fc 1982,William  Joho Jamuhuri fc Pemba 1985, Amour Azizi klabu ya Malindi ,Ahmed Kibapa Black Fighter 1980-1996 aliwahi kuutumikia timu ya Taifa ya Zanzibar, Waziri Sefu klabu ya malindi na Taifa ya Zanzibar miaka ya 1990, Mohamed Salum (marehemu) Kikwajuni na Taifa ya Zanzibar.

Majina yapo mengi haya ni baadhi ya wachezaji walikuwa wakilitendea haki nafasi ya kiungo wanapokuwa uwanjani ukweli tunajivunia kwa wachezaji hawa henzi zao sasa kizazi cha kinatakiwa kufata nyayo za wazee hawa kwenye nidhamu ya mpira wa Zanzibar ili kurudisha vipaji Zanzibar.