Waandishi wa habari Wametakiwa kufanya kazi  kwa kuzingatia maadili na sheria za kazi zao hususan katika kipindi cha Uchaguzi wa kitaifa unaotarajiwa kufanyika  2020.

Akizungumza na Zanzibar24 nje ya Sherehe za siku ya Waandishi wa habari zilizofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Rahaleo Mjini zanzibar.

Afisa Muandamizi wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shufaa Saidi Hassan amesema katika uchaguzi kunajitokeza mambo mengi hivyo si vyema kuaandika habari zisizo na ukweli ndani yake.

Amesema ni vyema  kwa Waandishi wa habari kufanya kazi kwa mashirikiano pamoja kufuata sheria na maadili ili kujiepusha na uvunjifu wa Amani Nchini.

Aidha ametowa wito kwa Waandishi hao kujiunga na Vyama vya Waandishi wa Habari ili waweze kunufaika na haki zao katika vyombo wanavyovifanyia kazi ikiwemo kutofanyishwa kazi kinyume na sheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kutoka chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar TAMWA Dk.Mzuri Issa amesema ni vyema kwa Waandishi wa Habari kuandika habari zao juu ya kuibua matatizo yaliopo katika makundi mbalimbali ikiwemo Wanawake na Walemavu.

Amesema waandishi watakapo andika habari zenye kuzingatia mahitaji ya wananchi zitaweza kuwawezesha wananchi kunufaika na mahitaji yao ya msingi kutoka kwa Viongozi wa Serikali pamoja na kuwawezesha wanawake kufika maendeleo.

Hata hivyo ametowa wito kwa Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia waandishi wa habari juu  ya maslahi madogo katika vyombo wanavyovifanyia kazi pamoja na kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria ambazo zinawakosesha uhuru wa kufanya kazi.

“Waandishi wamekuwa wakiekewa vikwazo katika kutekeleza majukumu ,na hata wengine kutishwa na kuambiwa wasitowee habari japo kuwa zina ukweli ndani yake jambo hiloo linawakoseshaa waandishi kufanya kazi zao”……alisema Dk.Mzuri

Nae Mkuu wa Taaluma kutoka chuo cha Uandiahi wa Habari  Zanzibar Rashid Omar Kombo amesema licha ya waandishi wa habari kufanya kazi kwa bidii bado wanakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo maslahi madogo kulingamisha na kazi zao.

Amesema Baadhi ya Wamiliki wa vyombo vya habari wamekuwa wakiwakosesha haki zao za msingi wafanya kazi wao ikiwemo kutowakipa kwa wakati jambo ambalo linaweza kuleta matatizo katika jamii.

Rashid amechukuwa fursa hiyo kuwashauri waandishi wa habari kufanya utafiti na uchunguzi wa mambo mbalimbali  ili kuimarisha maendeleo Nchini.

Katika maadhimisho hayo yaliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mihayo Juma N’hunga pia aliwasisitiza waandishi kutimiza wajibu wao katika habari wanazo ziandika hususan katika kipindi cha uchaguzi ili kuendelea kuipa heshima Tathnia ya Habari katika jamii.

Na:Fat-hiya Shehe Zanzibar24

fathiyashehe@gmail.com