Mafunzo ya uandishi wa habari za kiuchunguzi na jinsia kwa waadishi wa habari wanawake kutoka vyombo mbali mbali vya habari Zanzibar, yameanza leo Agosti 16, 2019 katika hoteli ya Zanzibar Paradise mjini Unguja.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo waandishi wanawake katika kuandaa na kuripoti kwa ufasaha habari za uchunguzi na jinsia nchini.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanawaleta pamoja waandishi 25 kutoka Unguja na Pemba wakiwemo wanawake 21 na wanaume 4. Wanaume wanashiriki kama viongozi wa Taasisi zao, na ni wafanya maamuzi kwa maeneo yao ya kazi. Wameshirikishwa kwa kuwa masuala ya jinsia yanahusisha pande zote mbili.

Mafunzo haya yatahitimishwa kesho na yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vy Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tanzania kwa kushirkiana na VIKES ambayo ni taasisi ya Habari ya Ufini kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya hi hiyo.

Washiriki wa Mafunzo ya uandishi wa habari za kiuchunguzi na jinsia wakimsikiliza mtoa mada.
Mshiriki wa mafunzo kutoka kikundi namba mbili akijibu maswala
Salome Kitomari mwenyekiti wa MISA Tanzania akitoa mada kwa waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali.