Waandishi wa habari Znzibar wametakiwa kuwa mstari wambele katika kuripoti kesi za udhalilishaji na kuzifuatilia mwanzo wake hadi mwisho wa hukumu wa kesi hizo.

Ushauri huo umetolewa na muendesha mashtaka wa Serikali Mohammed Iddi Saleh wakati akitoa mada juu ya mwenendo wakesi Mahakamani katika mafunzo ya waandishi wa Habari yaliyofanyika katika ukumbi wa Tamwa Zanzibar huko Tunguu Mkoa wa kusini Unguja

Awali akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa chama chama cha waandishi wa habaro wanawake Tanzania Tamwa  Dk. Mzuri Issa Ali amesema mchango wa vyombo vya Habari ni mkubwa katika kuripoti kesi za udhalilishaji hivyo waendelee kujitolea ili kuisaidia jamii.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Tamwa yaliyowakutanisha waandishi wa habari na waendesha mashtaka wa Serikali yenye lengo la kujadili mwenemdo wa Mahakama hakiza binaadamu na masuala ya kijinsia.

Na; Amina Omar.