Waandishi wa Habari wametakiwa kuripoti habari zilizokuwa na usahihi hususan habari zinazohusika na uchaguguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020 kwa lengo la kuimarisha amani nchini.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji kutoka katuo cha huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraji Mpatani wakati akiwasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa Habari yaliyowahusisha Asasi mbali mbali za kiraia juu ya suala zima la elimu ya kuripoti vyema matukio ya Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020 yaliyofanyika Ukumbi wa watu wenye ulemavu (UWZ) Weles Mjini Unguja.

Mkurugenzi Mtendaji kutoka katuo cha huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraji Mpatani wakati akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.

Amesema  nilazima Waandishi kutumia kalamu zao kwa kuzingatia maadili ya Uandishi kwa kuandika habari zililosawa napia zisizoleta athari kwa jamii.

Nae Mkurugenzi Ofisi ya Shirika la msaada marekani USAID anaeshuhulika na Utawala bora Jnnifer Horstall amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwaajili ya kuwawezesha wanahabari  kwa kuandika taarifa zao kwa kitaaluma zaidi kwa kuzingatia haki na usawa pamoja na maadili.

Mkurugenzi Ofisi ya Shirika la msaada marekani USAID anaeshuhulika na Utawala bora Jnnifer Horstall akiwapa mafunzo wanahabari.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Vijana (CYD) Bakari Omar Hamadi amesema wamekuwa wakiandaa vipengele mbali mbali  pamoja na kuwahusisha vijana kwa kuwapa mafunzo yanayohusiana na masuala ya Uchaguzi ili kuwajengea uelewa mzuri imeonesha kuwa  vijana wapo mstari wa mbele katika kupelekea machafuko.

Akitoa wito kwa Waandishi wa Habari Mkufunzi wa Vyombo vya habari internews Zanzibar Alalok Mayombo amewahusia wanahabari kuwa na uangalifu wa kuripoti habari zenye usawa kwani kipindi cha uchaguzi ni kigumu.

This image has an empty alt attribute; its file name is annna.jpg
Mkufunzi wa Vyombo vya habari internews Zanzibar Alalok Mayombo akiwapa mafunzo wanahabari zinazohusiana na tahadhari juu ya Uchaguzi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Internews kupitia kwa mradi wao wa BORESHA HABARI kwa ufadhili wa shirika la msaada Marekani (USAID)    

Na: Tatu Juma       `